Asubuhi ina mambo mengi na pengine uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita, ninazo hapa chini zile kubwa kubwa za leo zilizosikika redioni, kama zilikupita unaweza cheki na hizi nyingine kufidia.
Mahujaji waliofariki wafikia 4173, NEC yasema hakuna wizi wa kura, Magufuli asema mafisadi wajipange, vigogo UKAWA kuwekana kitimoto, NEC yasema matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka huu yatabandikwa vituoni, Rais wa serikali awamu ya tano safari hii kujilikana ndani ya masaa 72 na fomu ya Urais kuskaniwa jimboni.
Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva amesema safari hii kura zote zitahesabiwa kwenye vituo vya kupiga kura baada ya kupiga kura, mshindi wa Udiwani kutangazwa hapohapo huku matokeo ya Urais yatabandikwa katika vituo vya kila jimbo na pia kutangazwa kwenye Radio na TV hivyo hakuna kura zitakazoibiwa na wanasiasa waache kuwatisha wananchi kuhusu wizi wa kura kwenye Uchaguzi mkuu October 25.
Wananchi wa Tanga wafunga barabara ya msafara wa Edward Lowassa ili kumuona mgombea huyo, Polisi wasambaaratisha kura za Lowassa na Magufuli mtaani, kamatkamata ya wagombea Wabunge CHADEMA yafikia wanne, NEC imesema kuna vituo 72 ambavyo vimetengwa kwa ajili ya wapiga kura wenye matatizo ya ulemavu, CCM wamtimua mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Peter Elias kwenye kikosi cha waandishi wa habari kwenye msafara wa mgombea wao Dk. John Magufuli.
Mahujaji 112 wa Tanzania wawasili nchini kutoka Mecca huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imetoa majina ya watu 10 ambao mpaka sasa hawajulikani walipo.
Hapa chini nimekuwekea sauti ya uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast, karibu usikilize kwa kubonyeza play.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE