Imezoeleka wanaoshiriki mambo ya urembo ni mabinti ambao tayari wanajitambua na wenye uwezo wa kujibu maswali pale wanapokuwa wakihojiwa.
Hii imekuwa tofauti kwa Matilda Mackie mtoto aliyeshiriki mashindano hayo akiwa na wiki 5 tu tangu azaliwe huko Uingereza.
Mama wa mtoto huyo Jennifer alipeleka jina la mtoto wake kwa majaji wa shindano hilo la Kitaifa la urembo lililofanyika Glasgow mwezi uliopita na mwanaye kufanikiwa kuhika nafasi ya pili.
Mama huyo amesema nia ya kumshirikisha mwanaye huyo kwenye mashindano makubwa kama hayo ni kuweza kumshinda rafiki yake pamoja na kutimiza ndoto baada ya watoto wake wawili kufanya vizuri.
Amesema anajiona ni mama mwenye bahati kubwa baada ya watoto wake wengine Alexis na Maclan Mackie nao kufanikiwa kushiriki mashindano hayo na kufanya vizuri.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE