Wikiend iliyopita Diamond, Vanessa na Ommy Dimpoz wameiwakilisha vyema Tanzania katika tuzo za AFRIMMA zilizofanyika Marekani..Vanessa kazungumza kwenye 255 na kuwashukuru watanzania kwa kuwapigia kura, anajisikia faraja sana kushinda tuzo ya pili kimataifa, anasema imefungua kurasa mpya katika maiaha yake ya muziki.. pia amewataka wasanii wa kike wajitokeze katika sanaa hii.
Diamond baada ya kupata tuzo ya kwanza kati ya tatu alizopata aliidedicate kwa mtoto wake Tiffah..amesema ilikua ni moja ya ndoto zake na alitamani sana kupata tuzo hizo akiwa na mtoto,..jamaa anasema kuwa na mtoto kumemfanya azidi kufanya kazi kwa bidii sana ili mtoto wake aje kuishi maisha mazuri
Kundi la ‘mtu Chee’ linalomilikiwa na wasanii watatu Young Dee, Stamina na Country Boy limeonekana kuyumba.. kuna cover inasambaa mitandaoni ikiwa na teaser ya ngoma yao mpya lakini hayupo Young Dee na nafasi yake imechukuliwa na Young Killer..Country Boy kazungumza na kusema walikubaliana wote kutoa ngoma lakini Young Dee alionekana kutokuwa tayari na uongozi wake kumkataza kufanya kazi na kundi lake hilo..ikabidi wamuongeze Young Killer.
Jokate na team yake ya Kidoti walifanya tour katika shule mbalimbali, Jumamosi iliyopita ilikua hitimisho la ziara hiyo katika viwanja vya Jangwani..kwenye 255 leo Jokate amesema ilifanyika Jangwani na ilikua nzuri kwa kuwa wanafunzi wengi waliitikia wito . wanatarajia kufanya kila mwaka na kutakuwa na mambo mengi mazuri zaidi.
Vanessa, Diamond, Country Boy na Jokate wote wamesikika hapa kwenye 255…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,