Good Morning mtu wangu, Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za siku zinakufikia, hizi ni baadhi ya stori zilizoguswa kwenye Uchambuzi redioni.
Wataka Uspika sasa wafikia 21, Msaidizi wa Lowassa atimuliwa nchini, Zanzibar sasa vululu vululu, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akabidhi ofisi rasmi kwa Rais Dk. John Magufuli, Maduka ya dawa nje ya hospitali kufungwa na Rais Dk. John Magufuli atikisa kila kona.
Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kufunga maduka ya Dawa yanayozunguka Hospitali zote za Umma na vituo vya afya ili kupunguza mgongano wa kimaslahi na wizi wa dawa, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donald Mbando amesema wameanda utaratibu maalum wa maduka hayo ambayo rasimu hiyo ipo katika hatua za mwisho na MSD imeagizwa kufungua maduka ya dawa ndani ya hospitali ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama za huduma za matibabu.
Kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu Zanzibar umezua maswali makubwa kwa wananchi, wanaharakati Zanzibar wasema hatua ya kushindwa kuainisha vifungu vya Katiba ya Zanzibar kuhusu kufutwa kwa Uchaguzi Mkuu ni kitendo cha aibu… Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda azindua “#Sukuma Twende”, huduma ya kutoa malalamiko na ushauri bure kupitia simu ya mkononi ambayo itatumiwa na wananchi kufikisha malalamiko yao kwake.
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amemwagia sifa Rais Dk. John Magufuli kwa utendaji wake wa kazi wa kushitukiza, adai kitendo hico kimewapa msisimko mkubwa wananchi kwa kasi yake ya kazi… Vita ya kuwania Uspika wa Bunge imepamba moto huku Spika anayemaliza wakati wake Anna Makinda akishindwa kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo kutokana na ushauri aliopata kwa watu wake wa karibu.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE