Ni kawaida kwa wasanii wa muziki wa Pop R&B, na muziki wa Pop kwa ujumla kutumia dancers wakiwa kwenye live performances au kwenye matamasha mbalimbali ya muziki, na sababu kubwa ya kutumia dancers kwenye live performance ni kunogesha performance ya msanii husika… lakini hii kwa staa wa muziki wa Pop wa Uingereza, Adele imekaaje?
Nimetukana na interview moja aliowahi kufanya msanii huyo na ndani yake aliongelea vitu vingi sana ikiwa pia kugusia sababu ya kwanini kwenye Live Show zake nyingi hatumuoni akiwa na dancers wowote wale on stage…
>>> “sijawahi kuwa na dancers kutokana na aina muziki ninaoimba na aina ya mashabiki nilionao… japo kuna kipindi fulani cha tuzo za MTV VMA nilifikiria kufanya mbwembwe za aina hiyo stejini kwenye performance ya wimbo wa Someone Like You ila nikagundua kufanya hivyo itawavuruga mashabiki wangu ambao wengi wao hulipa hela kuja kukisikiliza kile ninachokiimba na sio kuona mbwembwe za dancers… pia aina ya muziki ninaoimba upo deep sana, itakuwa ngumu kutumia dancers, itaharibu vibe yangu na ya watu wanaokuja kunisikiliza…” <<< Adele.
Kwa sasa Adele anatamba na single yake mpya ‘Hello’ inayopatikana kwenye Album yake mpya ya 25, Album inayotarajia kuwa sokoni tarehe 20 November 2015 yani siku 3 kuanzia sasa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.