Kikao cha Bunge kwa leo November 19 2015 kimemalizana na kile ambacho kilikuwepo kwenye Ratiba ya Bunge… kwanza ilikuwa ni kutajwa jina la Waziri Mkuu pamoja na kumthibitisha, hilo limekamilika… kingine ilikuwa kumchagua na kumwapisha Naibu Spika wa Bunge, nalo limefanyika.
#MillardAyoUPDATES: Waziri Mkuu MAJALIWA KASSIM MAJALIWA amethibitishwa na Bunge kwa Kura 258 (73%) kuwa Waziri Mkuu awamu ya tano TZ.
— millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
Kila kitu kimekamilika, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa amethibitishwa na Bunge kushika nafasi hiyo na kesho ataapishwa…. Dk. Tulia Ackson Mwansasu pia amechaguliwa kushika nafasi ya Naibu Spika na ameapishwa leoleo. Kwenye sehemu ya Hotuba fupi ya Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, kuna hizi nukuu alichokisema baada ya Bunge kumthibitisha.
Kama umepitwa na Hotuba fupi ya Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim MAJALIWA baada ya kutangazwa, nanukuu kwenye #TWEETS alichokisema. — millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Namshukuru Mwenyezi MUNGU kumuongoza Rais JPM kuniteua, sikutegemea jambo hili ila nimelipokea’- #WaziriMkuuMAJALIWA
— millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Namshukuru sana Rais MAGUFULI kwa kuniamini na kunipendekeza kuwa Waziri Mkuu ‘- #WaziriMkuuMAJALIWA — millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Nampongeza Spika Job NDUGAI kwa kuchaguliwa kuongoza Bunge ambalo ni mhimili muhimu wa Serikali’- #WaziriMkuuMAJALIWA
— millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Nawashukuru Wabunge wote kwa kuridhia na kunipigia Kura, nawaahidi ushirikiano bila kujali vyama’- #WaziriMkuuMAJALIWA — millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Nawahakikishia kuwa tutafanya kazi kwa kushirikiana ili kuleta maendeleo kwa Wananchi na Taifa’- #WaziriMkuuMAJALIWA
— millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Naishukuru familia yangu na pia wapiga Kura wa Ruangwa kwa kunipigia Kura nikawa Mbunge wao’- #WaziriMkuuMAJALIWA — millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Naishukuru familia yangu na pia wapiga Kura wa Ruangwa kwa kunipigia Kura nikawa Mbunge wao’- #WaziriMkuuMAJALIWA
— millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Nawashukuru WaTZ wote, wana mchango mkubwa kufanya Rais akaniteua kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu’- #WaziriMkuuMAJALIWA — millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Nitafanya ziara kuona changamoto, maendeleo na kusikia mawazo na ushauri kutoka kwa WaTZ’- #WaziriMkuuMAJALIWA
— millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
#MillardAyoUPDATES: ‘Nawaombea Mwenyezi MUNGU awape nguvu, uwezo na aimarishe busara ili kuleta maendeleo TZ’- #WaziriMkuuMAJALIWA — millard ayo (@millardayo) November 19, 2015
Hii hapa video ya dakika 17 kutoka SIMU. Tv Waziri Mkuu alivyotangazwa na Hotuba yake ya kwanza.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.