Huu ujumbe umetoka kwa mke wa Rais wa Zimbabwe, Mama Grace Mugabe na umetolewa kwenda kwa warembo wote wanaopendelea vimini na suruali za kubana, anasema lolote baya likikukuta basi ujue umejitakia !!
Kama na wewe uko kwenye list ya wanaopendelea kuvaa hivyo, basi maneno ya Mama Mugabe yakufikie >>> “Kama unatembea huku umevaa kimini umeacha mapaja yako wazi, unawashawishi wanaume wakutamani.. hapo kama ikitokea umebakwa utalaumu? Huo ni ujinga wako mwenyewe.”– Mama Grace Mugabe.
Mama Grace Mugabe hakuishia hapo, ushauri wake ni huu hapa >>> “Mnapaswa kuvaa kama mimi au kama unavaa suruali isiwe ya kukubana sana…“
Ujumbe wake unapingana na madai ya kikundi cha Katswe Sisterhood, kilichopo Harare Zimbabwe ambao wamewahi kuandamana wakitaka wanawake kuruhusiwa kuwa na uhuru wa kujichagulia mavazi ya kuvaa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE