Hiki kimekua ni kipindi cha kutazama yote yaliyoahidiwa na Wagombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye nchi yetu ya Tanzania baada ya kutoka kwenye mbio za Uchaguzi Mkuu 2015,kwenye kasi ya Rais Magufuli ambayo kaanza nayo wapo wengine ambao wanapita na kasi hiyo hiyo.
Said Fella Mkurugenzi wa bendi ya Yamoto na Meneja wa kundi la Tmk Wanaume Family nae kaanza kutatua kero ambazo zimedumu kwa kipindi kirefu kwenye Kata yake ya Kilungule,kero ambazo alizihubiri kwenye majukwaaa wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Diwani,Kero hizo ni pamoja na Maji na suala la kupatiwa kituo cha Polisi.
Millardayo.com imepata nafasi ya kuzungumza na Said Fella>>mi’Jana tumeanza kuangalia kwenye visima ambavyo tumeanza kuvifanyia kazi,Leo tunaendelea na njia ambayo iliziba ya kwenda Yombo ndo tunaitengeneza na pia tumeanza Harambee mimi na wananchi wenzangu kumalizia kituo cha Polisi,Nadhani jioni ya Dec 01 tutakua tumemaliza awamu ya kwanza ya ujenzi wa kituo hiki’.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.