Mwezi September 2015, ilionekana vigumu kwa staa wa muziki wa R&B, Chris Brown kuingia Australia na kufanya show, sababu kuu zilikuwa mbili, utapeli na historia yake ya kupiga wanawake… lakini hiyo ilikuwa issue ya miezi mitatu iliyopita.. December hii mambo yapoje?
Serikali ya Australia imempatia staa huyo wa Virginia notice kuhusu kufikiria kuingia nchini humo, notice ambayo akiichukulia poa itamzuia kufanya tour yoyote Australia… Kufuatia notice hiyo, promoter wa Chris Brown hivi karibuni alichukua maamuzi ya kufuta tour mbili za msanii huyo, Tour ya Australia na tour nyingine ya New Zealand!
Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard wa Marekani, promoter wa Chris Brown alichukua time na kusema…
>>> “Mr. Brown na mapromoter wake wote wana matumaini kuwa tour hizo zitafanyika siku zijazo, licha ya hayo Mr. Brown angependa kuchua nafasi hii kuomba radhi kwa mashabiki wake na pia kuwashukuru kwa support yao kubwa wanayompa na anategemea kukutana na nyie kwenye tour nyingine zijazo“. <<< Nukuu kutoka Billboard.
Sababu kuu ya kumzuia Chris Brown kuingia kwenye nchi hizo na kufanya tour ni zile zinazoambatana na historia yake ya kumpiga na kumjeruhi aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Rihanna… ukiacha hayo Uingereza, Canada na New Zealand pia wamegoma kutoa visa yoyote kwa ajili ya msanii huyo kuingia kwenye nchi hizo.
Chris Brown alitakiwa kufanya shows kwenye miji ya Perth, Melbourne, Sydney na Brisbane kati ya December 9 na December 15.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.