Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema tayari limeshaanza kufanya mazunguzo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kufikia hatma ya akaunti yake kufungiwa. Kupitia kwa Afisa Habari wa Shirikisho hilo, Baraka Kizuguto, amesema wao kama TFF hawahusiki na kufungiwa kwa akaunti yao, bali serikali ndio chombo pekee kinachopaswa kuhojiwa kwanini TFF haijalipa kodi.
Kizuguto ameweka wazi kuwa kodi ambayo TFF wanadaiwa imetokana na mishahara waliyokuwa wanalipwa Makocha wa kigeni, tokea ujio wa Marcio Maximo pamoja na deni la kodi ya mchezo wa Brazil na Tanzania, uliofanyika mwaka 2010. Mishahara hiyo ilikuwa ikilipwa na serikali pia Kamati maalum ya serikali ndiyo ilihusika na mechi ya Taifa Stars na Brazil maana mapato yake hayakuingia kwenye akaunti ya TFF.
“ TRA wamezuia akaunti kwa madai kwamba kuna malimbikizo ya kodi ambayo yanafakia zaidi ya Bilioni 1.6 na deni hilo limetokana na malipo ya mishahara kwa makocha walioondoka, mapato yaliyopatikana kwenye mechi kati ya Taifa Stars na Brazil, kwa maana hiyo mapato na mishahara ya makocha hao ilikuwa haipitii TFF” >>>Kizuguto.
Shirikisho limesema kufungwa kwa akaunti hiyo kumesababisha timu ya Taifa ya Vijana Chini ya umri wa miaka 15 (U15) kushindwa kuendelea na ziara yake ya kutembelea Kigoma, Burundi, Rwanda, Uganda na mwisho Nairobi Kenya kutokana shirikisho kushindwa kugharamia.
TRA inaidai TFF zaidi ya bilioni 1.6 za kitanzania, ikiwa ni malimbikizo ya kodi kwa kipindi cha mwaka 2010 – 2013 huku akaunti iliyofungiwa ina jumla ya kiasi cha Shilingi milioni 300.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.