Uchambuzi wa magazeti redioni @CloudsFM umekupita? Inawezekana hukuzipata zote zilizoweka headlines kwenye magazeti ya Tanzania kama ilikupita hizi ni dakika 22 za zile zote kubwa za leo.
Rais Dk. John Magufuli jana aliwaongoza Watanzania kwenye kufanya usafi na kuwataka Watanzania wote kwa ujumla kujijengea utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara ili kuepukana na milipuko ya magonjwa kama Kipindupindu katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa DSM, Meck Sadiki na viongozi wa soko la Kariakoo kukutana naye siku ya jumatatu ofisini kwake ili kujadili namna ya kuboresha uendeshaji wa soko hilo pamoja na mazingira yake.
Rais mstaafu wa Serikali awamu ya nne, Jakaya Kikwete amevunja ukimya na kusema hajawahi agiza mtu yoyote asamehewe kodi ya Makontena bandarini, asisitiza hajawahi katika utawala wake kuagiza mtu yoyote anayestahili kulipa kodi asilipe.
Edward Lowassa asema ipo siku ataingia Ikulu kwa kupigiwa kura na Watanzania, asema hakuwa tayari kuingia Ikulu kwa damu ya watu na ana imani ipo siku atapigiwa kura na Watanzania kuwaongoza… Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA imewagomea kulipa kodi bila adhabu baadhi ya wailiki wa makontena ambayo yalitoroshwa kwenye bandari kavu bila kulipiwa kodi na kuwataka wafanyabiashara hao kuhakikisha wanalipa kodi na adhabu hiyo ndani ya siku saba.
Rais Dk. John Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 2336, kati yao wafungwa 117 wataachiwa huru huku wengine 2219 watabaki gerezani kutumikia kifungo cha sehemu iliyobaki.
Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ipo hapa chini, kusikiliza bonyeza play ikupeleke moja kwa moja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE