Baada ya mashabiki wa Ligi Kuu soka Tanzania bara kukosa burudani hiyo kwa wiki kadhaa kutokana na kusimama kwa Ligi ili kupisha maandalizi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria na kupisha michuano ya Kombe la Challenge lililokuwa linafanyika Ethiopia na Uganda kuibuka mshindi wa taji hilo, December 12 Ligi imeandelea kama kawaida na michezo sita imepigwa.
Mchezo ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ni mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Simba, huu ulikuwa ni mchezo ambao kwa upande wa Simba ulikuwa na presha kwa kocha wao mkuu Dylan Kerr ambaye kwa taarifa za chini ni kuwa uongozi ulikuwa hauridhishwi na mfumo wa ufundishaji wa kocha huyo.
Mchezo ulianza kwa Azam FC kupata goli la kuongoza dakika ya kwanza ya mchezo baada ya John Bocco kutumia vizuri pasi ya Farid Mussa na kupata goli la uongozi, Simba walitulia na kufanikiwa kusawazisha goli dakika ya 24 kupitia kwa mshambuliaji wao Ibrahim Ajib na kwenda mapumziko wakiwa 1-1. Kipindi cha pili Simba walirudi kwa kasi na Ibrahim Ajib kumzidi ujanja beki wa Azam FC Said Morad na kupachika goli la pili dakika ya 68 ila John Bocco akasawazisha goli hilo na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa December 12
- Stand United 0 – 2 Mwadui FC
- Mgambo JKT 0 – 0 Young Africans
- Kagera Sugar 1-1 Ndanda FC
- Mbeya City 2-2 Mtibwa Sugar
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.