Michezo

FC Barcelona yalazimishwa sare katika uwanja wake wa nyumbani Nou Camp (+Pichaz&Video)

on

Mechi za Ligi Kuu Hispania ziliendelea kama kawaida jumamosi ya December 12 kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali nchini humo, klabu ya FC Barcelona ambao ndio timu inayoongoza msimamo wa Ligi, ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Deportivo La Coruna katika uwanja wake wa Nou Camp jijini Barcelona.

4096

FC Barcelona ambao walikuwa na rekodi nzuri katika michezo yao ya Ligi Kuu msimu huu, walilazimishwa sare ya kufungana goli 2-2 dhidi ya Deportivo La Coruna na kuambulia kugawana point moja moja kwa pande zote mbili, licha ya kuwa FC Barcelona walikuwa na washambuliaji wao nyota Messi, na Suarez hawakufanikiwa kupata matokeo mazuri.

1967

Timu ya FC Barcelona ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli la kuongoza dakika ya 39 kupitia kwa Lionel Messi, wakati Deportivo La Coruna wakijiuliza namna ya kusawazisha goli hilo Ivan Rakitic akapachika goli la pili dakika ya 62, Deportivo La Coruna walianza kurudi mchezoni dakika ya 77 baada ya Lucas Perez kupachika goli la kwanza na baadae Alejandro Bergantinos dakika nne kabla ya dakika 90 kumalizika akapachika goli la kusawazisha kwa Deportivo.

Video ya magoli ya FC Barcelona Vs Deportivo La Coruna

https://youtu.be/_1UwWu1QmvQ

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments