Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Najua huenda stori nyingine zinakupita, hapa nimezikusanya zote zilizoguswa na #Tweets za #Magazeti Desemba 22, 2015, unazisoma zote kwa pamoja.
Serikali imesema itachukua hatua kali dhidi ya wamiliki wa vyuo ambao wanachelewesha mikopo kwa wanafunzi baada ya kupewa na bodi #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Waziri wa mambo ya ndani KITWANGA amepata kigugumizi kuweka hadharani orodha ya majina ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya #MTANZANIA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Abiria wanaosafiri kuelekea Mikoa ya Kaskazini jana nusura wapigane wakigombea tiketi katika kituo cha mabasi ya Mikoani Ubungo #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Rais MAGUFULI jana amekutana na aliyekuwa mgombea Urais wa Z’bar Maalim SEIF Ikulu na kufanya naye mazungumzo kwa saa 2 #MTANZANIA #DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
49% ya matokeo ya uchunguzi wa makosa ya DNA yanayowasilishwa kwa Mkemia mkuu kwa mwaka yanaonekana baba si mzazi halali wa mtoto #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia askari sita kwa tuhuma za mauaji #MagazetiDEC22 https://t.co/3eRlumhjsl
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
CHADEMA kimemuomba rais MAGUFULI kuingilia kati mgogoro wa uchaguzi wa Mameya katika manispaa za Ilala na Kinondoni #MTANZANIA #DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Waziri Mkuu MAJALIWA amepiga marufuku chakula cha msaada kutumiwa kutengeneza pombe za kienyeji,atakayekamatwa atachukuliwa hatua #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Familia 16 za Wilaya ya Chemba, Dodoma zimelazimika kukimbia makazi yao kutokana na hofu ya mtikisiko wa ardhi #MTANZANIA #DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Wakimbizi wanaotokea Burundi wakikwepa machafuko wamezidi kufurika katika kambi ya Kibondo iliyopo Kigoma na kufikia 60,000 #MTANZANIA DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
80% ya watoto waliolazwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya matibabu mbalimbali wanakabiliwa na utapiamlo #MTANZANIA #DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
RC Mwanza amesema hatafikiria mara mbili kuwafukuza kazi wakuu wa shule za msingi watakaowatoza fedha wanafunzi wanaoanza shule #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Mahabusu sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji jana waligoma na kukaa katikati ya barabara wakishinikiza kesi zao zisikilizwe #MTANZANIA DEC
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Balozi SEFUE amevitaka vyuo na taasisi za elimu nchini kuhakikisha vinatoa mafunzo bora yanayoendana na mahitaji ya soko la ajira #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Wafanyabiashara soko la Kilombero Arusha wamesema kupanda kwa bei ya vyakula kipindi cha sikukuu kumechangiwa na uzalishaji mdogo #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Kiongozi wa upinzania Kenya Raila Odinga amemtaka Rais Kenyatta kumuamuru naibu wake RUTO achunguzwe ili kubainisha utajiri wake #MTANZANIA
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Rais KAGAME wa Rwanda amempongeza Rais MAGUFULI kwa hatua anazozichukua hasa utendaji kazi katika bandari ya Dar es salaam #MWANANCHI #DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Bohari ya dawa MSD imesema maduka yake yatatoa huduma kwa wagonjwa wenye vyeti vya daktari pekee #MWANANCHI #DEC22 https://t.co/3eRlumhjsl
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Kikosi maalum cha kupambana na ujangili kimemtia mbaroni mlinzi wa mfalme wa Qatar kwa kusafirisha fuvu la twiga kwenda Uarabuni #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Waziri ANGELLA KAIRUKI amesema waajiri wasitegemee Serikali kuruhusu kuendelea kutoa mikataba kwa watumishi wanaostaafu #MWANANCHI #DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Waziri wa Nishati na Madini Prof.MUHONGO amesema ataanza kuwatimua wafanyakazi wazembe wasiokuwa na tija ktk muda wa siku90 zijazo#MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
SUMATRA imelazimika kutoa vibali vya wiki moja kwa mabasi ya Mikoa ambayo haina abiria wengi kwenda Mikoa ya kanda ya Kaskazini #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
CHADEMA kimemtaka Rais MAGUFULI atumbue majipu yaliyosababisha dosari kujitokeza kwenye chaguzi za viongozi wa Halmashauri nchini #MWANANCHI
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Kasi ya uchapa kazi ya Rais MAGUFULI imewatisha baadhi ya wanasiasa,wafanyabiashara waliokuwa wakinufaika na mfumo wa kifisadi #GazetiTAZAMA

CCM yaibuka kidedea majimbo ya Ludewa na Masasi katika uchaguzi mdogo wa nafasi za Ubunge, mgombea wa CUF akataa matokeo #MWANANCHI DEC22
— millard ayo (@millardayo) December 22, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.