Headlines za wanasoka wa kibongo kuulizwa kuhusu lini watastaafu kucheza soka zimekuwa zikiandikwa sana mitandaoni na hata kwenye vyombo vya habari, alianza kusikika nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na klabu ya Dar Es Salaam Young African Nadir Haroub Canavaro kuwa kacheza kwa muda mrefu, hivyo lini atastaafu?
Canavaro kupitia gazeti la habari leo alijibu kuwa kuhusu suala la kustaafu kucheza timu ya taifa anaweza kufikiria baada ya miaka mitatu, lakini kama atafanya hivyo ataendelea kuichezea klabu yake ya Yanga kama kawaida. Baada ya hapo millardayo.com ilipata bahati ya kukutana na Abdi Kassim Babi na kumuuliza kama ana mipango ya kuustafu?
“Muda wa kustaafu haujafika, nafikiria kufanya hivyo baada ya miaka mitatu na nikistaafu bado nitaendelea na kuichezea Yanga, na ikitokea nimeondoka Yanga basi ndio mwisho wa jina langu kusikika kwenye soka, kwani sifikirii kuichezea timu nyingine baada ya hapo,” >>> Canavaro
Babi ambaye amewahi kuvitumikia vilabu vya Mtibwa Sugar, Yanga na Azam FC kwa sasa anacheza soka katika klabu ya UiTM ya Malaysia na yupo likizo Tanzania baada ya msimu wa Ligi Kuu Malaysia kumalizika. Majibu Babi ndio haya kuhusu mipango yake ya kuustaafu soka.
“Kwa uwezo wa mungu mimi kuustaafu soka ni baada ya miaka saba yaani hadi mwaka 2022, mpira napenda najiona bado na nguvu na naweza ndio maana bado nina malengo na soka. Kwa sababu kucheza soka hakurudi nyuma ndio maana naimalizia vizuri kwani ikiisha imeisha tu” >>>Abdi Kassim Babi
Hii ni sauti ya Abdi Kassim akianza kwa kueleza mechi ambayo hawezi kuisahau
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.