Wiki kadhaa nyuma kiungo wa kimataifa wa Ujerumani anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Mesut Ozil alikuwa anatajwa kama assist King, ikiwa na maanakuwa yeye ndio mtaalam wa assist au mkali wa assist, lakini February 4 stori kutoka sokkaa.com inaripoti kuwa amezidiwa na kuwa nafasi ya pili sawa na Neymar wa klabu ya FC Barcelona. Hii ndio TOP 6 ya wachezaji wanaoongoza kwa assists.
6-Luis Suarez- Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania ambaye usiku wa kuamkia February 4 alifunga goli nne dhidi ya Valencia na kufikisha jumla ya magoli 35 katika michezo 33, Suarez yupo nafasi ya sita kwa kutoa jumla ya assist 11.
5- Angel Di Maria- Huenda klabu ya Man United na mashabiki wake hawafurahii hili kutokana na mchezaji huyo kahama klabu yao, Di Maria anatajwa kufanya vizuri ndani ya klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa. PSG hadi sasa hawajapoteza mchezo wowote msimu huu, lakini good news nyingine ni kuwa Di Maria ana jumla ya assist 12 na magoli 12.
4- Kevin De Bruyne kutoka klabu ya Man City na timu ya taifa ya Ubelgijia, amekuwa na mchango mkubwa msimu huu ndani ya klabu ya Man City msimu huu, licha ya kuwa ana assist sawa na Di Maria, De Bruyne amewekwa nafasi ya nne.
3- Mesut Ozil- ndio alikuwa kinara wa kutoa assist nyingi katika mechi moja, kwani aliweka rekodi ya kutoa assist zaidi ya moja katika mechi nne mfululizo, Ozil kwa sasa bado ana assist 16 sawa na Neymar.
2- Neymar- amekuwa nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya assist 16 sawa na Ozil ila yeye kafunga jumla ya goli 21, katika mechi 28 za mashindano yote.
1- Henrikh Mkhitaryan wa Borussia Dortmund kwa sasa ndio unaweza muita assist king kwa bara la Ulaya, ana jumla ya assist 17 na goli 17, hizo ni assist za jumla ya mashindano yote aliyocheza hadi sasa msimu huu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwapia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagramna YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.