Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo kwa klabu ya Simba kushuka uwanja wa Taifa Dar Es Salaam kuikabili Mbeya City katika mchezo wao wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2015/2016.
Simba ilishuka uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ikiwa haina kumbukumbu ya kuwahi kuifunga Mbeya City katika uwanja huu zaidi ya sare na kupoteza, hivyo Simba kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Mbeya City, inakuwa imeweka rekodi ya kuifunga Mbeya City kwa mara ya kwanza uwanja wa Taifa Dar na mara ya pili katika historia.
Magoli ya Simba yalifungwa kipindi cha pili, baada ya Awadh Juma kupiga shuti na kupanguliwa na golikipa wa Mbeya City Kalyesebula na Daniel Lyanga kupachika goli la kwanza kwa Simba dakika ya 75, Simba walifunga goli la pili dakika ya 90 kupitia kwa Ibrahim Ajib na kujihakikishia kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi, mbele ya Yanga na Azam FC kwa tofauti ya point moja.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE