Aliyekuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’, Harry Kitilya, Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi benki ya Stanibic tawi la Tanzania pia ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare wamefika Mahakama kuu leo ili kusikiliza rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.
Upande wa utetezi umedai kuwa mahakama hiyo aina mamlaka ya kusikiliza rufani kwa kuwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu haikumaliza kusikiliza kesi hiyo lakini upande wa serikali umesema haki wanayo kwa sababu shitaka la nane limeshamalizika. Mahakama Kuu imeeleza kuwa kesho ndio itatoa uamuzi wa Rufani hiyo kama isikilizwe mahakamani hapo au la.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIKOSA YA ZITTO KABWE KUHUSU UTUMBUAJI WA MAJIPU NA BUNGE KURUSHWA LIVE? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI