May 06 2016 Rais Magufuli amezungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika mikoa ya Singida na Manyara wakati waliposimamisha msafara wake uliokuwa ukitoka Dodoma kwenda Arusha.
Rais Magufuli ameyazungumza haya matatu na kutoa maagizo kwa wafanyabiashara wanaoficha sukari kuanza kuisambaza mara moja, vinginevyo serikali itachukua hatua kali.
‘Wale wote waliokuwa wameficha sukari waiachie, wasipoiachia sukari, huwezi kuificha kama sindano, nimeshaagiza vyombo vya dola, vikague magodown yote atakayekutwa na sukari ameificha, yule ni mhujumu uchumi kama wahujumu wengine, asije akanilaumu, asijee-akanilaumu, na ninasema kwa dhati’.
‘wewe mfanyabiashara uliyepata nafasi ya Tanzania kuleta bidha za sukari, halafu unanunua unakwenda kuficha ili kusudi wazee hawa wahangaike, ili mwezi mtukufu wa Ramadhani utakapoingia watu wakose sukari, dawa yao ninayo’.
Rais Magufuli amewaondoa shaka watanzania juu ya upungufu wa sukari, kuwa serikali imeagiza sukari kutoka nje ya nchi ambayo itasambazwa kwa wananchi kwa bei nafuu ili kufidia upungufu uliopo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA HII YA WAZIRI MKUU KUONGEA BAADA YA UPUNGUFU WA SUKARI KUJITOKEZA? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI