Baada ya siku saba ambazo wananchi wa Dar es salaam kutumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka bure, leo May 16 2016 utaratibu wa kulipia umeanza ambazo baadhi ya changamoto zimejitokeza ambazo ni pamoja na umeme kukatika kwenye vituo vya kukatia tiketi na kusababisha huduma kusimama pia foleni wakati wa ukataji wa tiketi na upatikanaji wa chenji.
Video hii hapa chini ni Majira ya asubuhi ambapoi abiria waliokuwa kwenye kituo cha ubungo maji na rombo wamekumbana na tatizo la kusumbua kwa mtandao ambao unatumika kutoa tiketi, abiria waliambiwa wasogee kituo cha mbele cha ubungo terminal kupata huduma hiyo.
Video hii hapa chini inaonyesha abiria waliokuwa kwenye foleni kituo cha mabasi yaendayo haraka Nyerere Square wakizozana na muuza tiketi baada ya umeme kukatika na huduma ya kutoa tiketi kusimama mpaka umeme utakaporudi au abiria kwenda kituo cha mbele cha kisutu.
A video posted by millard ayo (@millardayo) on
ULIKOSA NAULI ZA MABASI MAPYA YA HARAKA ZILIPOTAJWA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE