Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini
Moja ya story kubwa June 02 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘Kina Zitto , Lissu, Mdee kukatwa mshahara, posho’, gazeti hilo limeripoti kuwa wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa bungeni watakumbana na kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.
Gazeti hilo limesema wabunge hao ambao jumatatu walisimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Halima Mdee, Ester Bulaya, John Heche na Godbless Lema.
Gazeti hilo limeongeza kuwa adhabu hiyo iliyotolewa kama azimio la bunge baada ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe kutokana na kuomba muongozo wa kiti cha Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi
Habari zilizopatikana bungeni na kuripotiwa na Gazeti hilo la Mwananchi zilieleza kuwa wabunge hao watakumbana na kanuni ya bunge ya 75 ambayo inahusika na masharti ya mbunge aliyesimamishwa kazi’. Akizungumzia na gazeti hilo Zitto alisema hajasikia taarifa hizo za kukatwa mshahara kwa kuwa hajapewa barua inayoeleza mambo hayo wala kusimamishwa bunge.
#MWANANCHI Wabunge saba waliosimamishwa watakumbana na kibano kingine cha kukatwa mshahara, posho kwa kipindi chote pic.twitter.com/HVlVmmAG1a
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#MTANZANIA Serikali imetuma kikosi cha ulinzi Tanga kikiongozwa na JWTZ kuwasaka wanaodaiwa kuwa majambazi pic.twitter.com/dWahZJHKnY
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#MTANZANIA Mtikisiko unaweza kuikumba sekta ya afya baada ya miradi iliyokuwa inafadhiliwa na USAID kufika mwisho pic.twitter.com/Y5H5vZmV0a
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#NIPASHE Miili ya wawili waliozikwa Shinyanga imekutwa imeliwa baada ya kufukuliwa na wanyama wanaodhaniwa kuwa fisi pic.twitter.com/lKIaH8szYZ
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#NIPASHE Agizo la Rais Magufuli la kutoa bure EFD limeanza kutekelezwa, wafanyabiashara 5,703 Dar kugawiwa pic.twitter.com/Z7pmVJr4Sk
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#NIPASHE Polisi K'ndoni imeandaa mpango maalumu wa kutunza kumbukumbu za taarifa za wahalifu ikiwamo kupigwa picha pic.twitter.com/vWPtt2lDOS
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#MWANANCHI Mauaji ya watu wanane waliochinjwa Tanga imebainika wauaji waliwachinja kuanzia sehemu ya chini ya kisogo pic.twitter.com/l3BaTZTY9n
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#MWANANCHI Wanafunzi walioandamana UDSM wakishinikiza malipo yao, huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu pic.twitter.com/SBftSeB9w6
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#JamboLEO Serikali imetenga sh bil 10 kwa ajili ya kukarabati kiwanja cha Ndege cha Mtwara pic.twitter.com/sBDMJ9BGNn
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#JamboLEO Polisi Ilala imesema watu 40 wamepoteza maisha kutokana na ajali 37 kati ya 848 Jan hadi May 2016 pic.twitter.com/zvmGzxmgAG
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#NIPASHE Bibi anayekadiriwa kuwa na miaka 70 akutwa usiku ktk nyumba ya waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi, Nchemba pic.twitter.com/u9QuzGBNMO
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
https://twitter.com/millardayo/status/738247946253258752
#NIPASHE Ripoti ya WHO inaonyesha kuwa baadhi ya majiji mengi machafu zaidi duniani yako nchini Nigeria pic.twitter.com/G0RfRKZA26
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#NIPASHE Naibu Spika amewataka wasioridhika na uamuzi wa kiti cha Spika kukata rufaa kamati ya kanuni za bunge pic.twitter.com/Si9oKIcGrX
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#NIPASHE Serikali imesema kutokana na uwezo mdogo wa kifedha kidato cha nne hawatajiunga na JKT pic.twitter.com/y3bOdVkUNm
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
#MWANANCHI Upinzani wamewasilisha kwa spika hoja ya kumwondoa Naibu Spika, Dk Tulia kwa kutokuwa na imani naye pic.twitter.com/VXfuQrwD2c
— millardayo (@millardayo) June 2, 2016
ULIKOSA HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA JUNE 2 2016? NAIBU SPIKA AWAJIBU UKAWA, JK ASEMA BILA MISAADA HATUENDI, UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE