fB insta twitter

Baada ya wabunge saba wa upinzani kusimamishwa sasa kukumbana na kibano kingine

on

Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini

Moja ya story kubwa June 02 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘Kina Zitto , Lissu, Mdee kukatwa mshahara, posho’, gazeti hilo limeripoti kuwa wabunge saba wa upinzani waliosimamishwa bungeni watakumbana na kibano kingine cha kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.

Gazeti hilo limesema wabunge hao ambao jumatatu walisimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa muda tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Halima Mdee, Ester Bulaya, John Heche na Godbless Lema.

Gazeti hilo limeongeza kuwa adhabu hiyo iliyotolewa kama azimio la bunge baada ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe kutokana na kuomba muongozo wa kiti cha Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa uamuzi

Habari zilizopatikana bungeni na kuripotiwa na Gazeti hilo la Mwananchi zilieleza kuwa wabunge hao watakumbana na kanuni ya bunge ya 75 ambayo inahusika na masharti ya mbunge aliyesimamishwa kazi’. Akizungumzia na gazeti hilo Zitto alisema hajasikia taarifa hizo za kukatwa mshahara kwa kuwa hajapewa barua inayoeleza mambo hayo wala kusimamishwa bunge.  

ULIKOSA HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA JUNE 2 2016? NAIBU SPIKA AWAJIBU UKAWA, JK ASEMA BILA MISAADA HATUENDI, UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments