Wanafunzi 316 waliosimamishwa masomo chuo kikuu cha St. Joseph Kampasi ya Dar es salaam, walifungua kesi ya kuomba kibali cha kuwakilisha wenzao mahakamani pamoja na chuo kusitisha masomo wakati kesi ya msingi ikiendelea kusikilizwa.
Kesi hiyo imetajwa leo June 10 2016 Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam ambapo imetoa kibali kwa wanafunzi kufungua kesi dhidi ya chuo hicho na Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU’
Akitoa ufafanuzi wakili wa walalamikaji, Emmanuel Muga amesema……..>>>’hii kesi ina utaratibu kwa sababu mpo wengi wanafunzi 316 ikiwa ni watu wengi inabidi upande kibali cha mahakama ili ufungue hiyo kesi na hiyo kesi itawakilishwa na watu wachache yaani watu wanne tu lakini ili watu wanne wawakilishe wenzo wote lazima mahakama itoe kibali’
Katika madai ya msingi, walalamikaji wanadai fidia ya miaka mitatu waliokaa chuoni hapo dhidi ya chuo na Tume ya vyuo vikuu Tanzania ‘TCU’.
ULIKOSA WAZIRI WA ELIMU ALIVYOENDA MWENYEWE CHUO CHA MT. JOSEPH DSM BAADA YA KUPATA TAARIFA ZAO? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE