Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yalioandikwa ni huu utafiti wenye kwenye gazeti la Habari leo yenye kichwa ‘Siri ya kuzuia udahili vyuo vikuu hadharani”
#HabariLEO Imebainika baadhi ya vyuo vikuu hutoa elimu bila kuzingatia sifa, idadi kubwa ya wanafunzi kuliko walimu pic.twitter.com/UyZARraXUf
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
Wakati serikali imezuia baadhi ya vyuo vya elimu ya juu kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo wa 2016/2017, kasoro zilizosababisha zuio hilo zimebainika.
Uchunguzi wa gazeti Habari leo uliofanywa kwa takribani wiki mbili, ulibaini baadhi ya vyuo nchini hutoa elimu bila ya kuzingatia sifa, huku baadhi vikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi kuliko walimu, kutokuwa na maabara na majengo muhimu, kuwa na wanafunzi wasio na sifa, kuwa na wakuu au makamu wakuu wasio na sifa.
Ofisa uhusiano wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), Edward Mkaku aliliambia gazeti hilo siku chache zilizopita kuwa serikali kupitia TCU ilikua imeunda Tume Maalum ili kuchunguza uendeshaji wa vyuo vikuu nchini.
Alisema mara baada ya tume hiyo kukamilisha kazi yake, TCU itakua katika nafasi nzuri zaidi ya kueleza kile kilichobainika katika ukaguzi huo na hatua zitazochukuliwa na serikali.
#NIPASHE Zitto asema ukali wa Mwenyekiti CCM, JPM ni faida kwa mfumo wa vyama vingi kwa sababu upinzani utaimarika pic.twitter.com/M82wpZCrHU
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#MWANANCHI TBS imefungua ofisi za kanda Arusha, Mwanza na Mbeya ikiwa ni jitihada za kuongeza ufanisi na huduma bora pic.twitter.com/eSFRWqTisI
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#HabariLEO Safari ya nchi kuhamia Dom yaanza, Ihumwa kujengwa majengo ya Wizara, maeneo ya biashara nayo yaainishwa pic.twitter.com/JML8GwPiII
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#HabariLEO Uhaba wa sukari K'njaro, Arusha, Manyara, Singida umekwisha baada ya kiwanda cha TPC kuzalisha tani 8,825 pic.twitter.com/C8iEigAbKz
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#HabariLEO TRA Lindi imekusanya bil 6.4 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 pic.twitter.com/BvlrGJNY9L
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#JamboLEO Waziri Ndalichako amesema kazi bado pevu TCU kutokana na madudu kuendelea kuonekana vyuoni pic.twitter.com/GJUr4n2vA0
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#JamboLEO Sakata la sukari bado bichi yabainika wakulima Turiani wamekisusa kilimo cha miwa, wageukia mazao mengine pic.twitter.com/u4ce93gB5g
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#JamboLEO Wapigania uhuru wapendekeza mtu wa kimrithi Rais Mugabe kuwa ni makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa pic.twitter.com/kmQ1oVcLi9
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#JamboLEO TRA yaandaa mfumo mpya wa utoaji tiketi za kielektroniki kwa wasafiri wa mabasi yaendayo mikoani pic.twitter.com/pBHgHR4KTZ
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#TanzaniaDAIMA Baada ya Makamba kudai Gwajima alizua uongo dhidi ya JK, Gwajima asema hawezi kumjibu si saizi yake pic.twitter.com/vYvhhq0kEU
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#TanzaniaDAIMA Waziri Ndalichako amesema sekta ya elimu imekosa uadilifu ndio maana imekuwa na upungufu mkubwa pic.twitter.com/IlxgaO2vLw
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#UHURU Wiki hii Serikali kuweka wazi majina ya walionufaika na mikopo elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha pic.twitter.com/RrZhJdZduB
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#UHURU Serikali kutoa hatimiliki zaidi ya 25,000 Kimara, Saranga Dar ikiwa ni hatua ya kurasimisha makazi holela pic.twitter.com/jYKjna0Pfb
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#RaiaTANZANIA Waziri Mwalimu amesema alichopiga marufuku ni NGOs kununua na kusambaza vilainishi kwa 'mashoga' pic.twitter.com/NiQMJU73tz
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#RaiaTANZANIA Mnyika amesema vyama vinavyoshabikia CCM havifai kwenye orodha ya hekaheka za vuguvugu la mabadiliko pic.twitter.com/7AklcpvKmB
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#NIPASHE Uwanja wa ndege kupewa jina la Cristiano Ronaldo, uwanja huko kisiwa cha Madeira alipozaliwa nyota huyo pic.twitter.com/ONp2IM2nsg
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
#MWANANCHI TRA Hai na Siha K'njaro imevuka lengo kwa kukusanya bil 2.51 kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 pic.twitter.com/wWaVpEKNyM
— millardayo (@millardayo) July 25, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JULY 25 2016 KUTOKA AYO TV?UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI