Leo August 15 2016 Tume ya uchaguzi nchini Zambia imemtangaza aliyekuwa rais wa Zambia, Edgar Lungu kuwa mshindi wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama cha Patriotic Front kwa awamu ya pili.
Lungu alijipatia asilimia 50.35 ambazo ni kura 1, 860, 877 na Kumshinda mpinzani wake Hakande Hichilema wa chama cha United Party for National Development ambaye amepata asilimia 47.67 ambazo ni kura 1, 760, 347
Imeelezwa kuwa awali chama chake cha UNDP kilijiondoa katika shughuli ya uhakiki kura akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu.
Rais wa Zambia Edgar Lungu ametangazwa mshindi matokeo ya uchaguzi wa urais kulingana na matokeo rasmi ya uchaguzi pic.twitter.com/gy69YlZpRW
— millardayo (@millardayo) August 15, 2016
ULIKOSA KUITAZAMA VIDEO YA WATUMISHI 99% WA BUNGE KUHAMIA DODOMA NA 1% KUBAKI DSM? UNAWEZA KUIONA VIDEO NIMEKUWEKEA HAPA CHINI