Baada ya Jeshi la polisi Arusha kumshikilia Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, Lengai Ole Sabaya wakidai wamepata malalamiko kwa wananchi kuwa amekuwa akitumia kitambulisho cha usalama wa taifa kutapeli.
Leo September 19 2016 kiongozi huyo wa UVCCM amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Arusha na kusomewa mashtaka mawili ya kughushi kitambulisho cha usalama wa Taifa na kukitumia kwa utapeli.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Gwantwa Mwankunga amemuachia mtuhumiwa wa dhamana ya watu wawili ambao kila mmoja alitakiwa kutoa sh. milioni 3 na kesi imeahirishwa hadi october 5 mwaka huu. Akizungumza nje ya mahakama hiyo Lengai Ole Sabaya amesema…….
>>>Mahakama imenipa nafasi ya kudeal na watu ambao walisambaza kwa muda mrefu sana uzushi ambao hawakuwa na ushahidi nao kwa hiyo walicheza dakika 45 za kwanza dakika 45 za pili zitachezwa ndani ya jengo hili tukufu ‘mahakama’ tutapata muda wa kuwaumbua mchwa walioko ndani ya CCM wanaoshirikiana na upinzani na walioko Arusha’
ULIKOSA HII YA KIONGOZI UVCCM KUDAIWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA TAIFA KWA UTAPELI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI