Mtu wangu unaambiwa Vodacom Tanzania wakishirikiana na Benki ya CBA walizindua promosheni kubwa inayojulikana kama “Jiongeze na M- Pawa’‘ ambayo inawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia zawadi ya fedha taslimu.
Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100 na washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja.
Promosheni hiyo ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa 9 itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktober, 2016.
Sasa Vodacom wamechezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Hadi sasa washindi 2,800 wameongezea mara mbili ya akiba zao za M-Pawa washindi 14 wameshinda milioni 1 kila mmoja na washindi 2 wamejishindia milioni 20 mshindi wa jumla wa shilingi milioni 100 atapatikana mwezi wa October.
ULIKOSA HII YA VODACOM KUKABIDHI MIL 20 KWA MSHINDI WA PROMOSHENI YA KAMATA MPUNGA? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI