Kampuni ya vifaa vya mawasiliano ya AT&T Inc imetangaza kukubaliana na kampuni ya Time Warner Inc deal ya dola za Marekani kiasi cha Bilioni 85.4, ikiwa ni malipo ya kuvinunua vituo vya TV vinavyotamba duniani ikiwemo CNN kwa lengo la kufanya uwekezaji mkubwa zaidi.
Hii inatajwa kuwa itakua deal ya kibiashara kubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye vyombo vya mawasiliano na habari duniani. Kwa mujibu wa Huffington Post kampuni ya AT&T itakua na umiliki wa chaneli zote za cable TV za HBO, kituo cha habari cha CNN, studio za filamu za Warner Bros pamoja na vifaa vyote vilivyo chini yake.
AT&T watatakiwa kulipa kiasi cha dola za Marekani $107.50 kama charges za hisa kwa kampuni ya Time Warner, ikiwa ni mjumuisho wa pesa taslimu na malipo ya muda mrefu ambayo yatafikisha juma ya dola Bilioni 85.4. AT&T wamesema watakua wamekamilisha malipo yote ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017.
ULIPITWA NA TAARIFA YA MIKATABA 22 ILIYOSAINIWA KATI YA MOROCCO NA TANZANIA? NIMEKUWEKEA HAPA