Wakati Rais Magufuli akitimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani Leo November 04 2016 amekutana na waandishi wa habari IKULU Dar es salaam na kujibu maswali mbalimbali, moja ya swali, lililoanza kuulizwa lilimtaka Rais Magufuli kusema namna anavyojitathmini katika mwaka wake mmoja wa uongozi. Rais Magufuli amejibu…
>>>Umeniuliza swali gumu, ni vizuri watu kukutathmini kuliko kuliko wewe mwenyewe kujitathimini, nilipokuwa nimechaguliwa yapo tuliyokuwa tumeyaahidi, nilitoa hotuba ya kwanza bungeni nilisema nataka kuwa na serikali ya hapa kazi tu, kila mtu afanye kazi, nahisi nimetimiza hayo