Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Magazeti yote ya Tanzania leo Nov 21 2016 na habari zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho pic.twitter.com/wclGp02PIJ
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MWANANCHI 1.Katiba Mpya 2.Maafa ya Kagera 3. Maamuzi ya Haraka 4. Mikutano ya Siasa 5. Sakata la Zanzibar 6. Bunge Live 8. Matamko 9. Ukata pic.twitter.com/4uC1KpMpv5
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
Serikali ya Awamu ya Tano imefanya vizuri katika mwaka wake wa kwanza, ikifanikiwa kurejesha nidhamu ya kazi kwa kiasi kikubwa, kupambana na ufisadi, kukusanya mapato ya Serikali na kuwawajibisha bila aibu viongozi na watumishi wa umma.
Ununuzi wa ndege mbili, malipo yaliyofanikisha awamu ya pili ya mradi wa umeme wa Segerea, kuanzisha mahakama ya mafisadi, kuzuia matumizi yasiyo ya lazima kwa kufuta sherehe za maadhimisho ni kati ya mambo yaliyofurahiwa na wengi.
Lakini, wakati Rais John Magufuli na Serikali yake wakianza mwaka wa pili, baadhi ya wasomi na wanasiasa wamemshauri Rais Magufuli afanyie kazi mambo 10, likiwamo la mchakato wa Katiba mpya ambalo alisema si kipaumbele chake.
Mbali ya Katiba, wachambuzi hao walitaja mambo mengine muhimu yanayopaswa kufanyiwa kazi kuwa ni kuangalia uwezekano wa kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, hali ya siasa Zanzibar, kuheshimu sheria wakati wa kuwajibisha watumishi, kuruhusu uhuru wa mihimili ya nchi, kuruhusu demokrasia, kuruhusu shughuli zote za Bunge kuonyeshwa moja moja na vituo vya televisheni na redio na kuepuka kauli tata.
“(Rais Magufuli) Amefanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa, kuwafanya watu wapende na kuheshimu kazi. Sasa atakavyomaliza na kuondoka, haya yote yataachwa ikiwa hatasimamia mchakato wa Katiba mpya,” -Dk Hellen Kijo-Bisimba.
*Katiba Mpya*
Ilani ya CCM inazungumzia mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa kipindi cha 2010-2015 kuwa ni pamoja na mchakato wa kuandika Katiba mpya kuendeshwa na kufikia hatua ya kupigia kura Katiba Inayopendekezwa baada ya kupitishwa na Bunge maalumu.
Akipokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu Juni 23, Magufuli alisema mambo fulani yataongezeka katika Katiba Inayopendekezwa, lakini Novemba 4 alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari alisema hakuwahi
kuzungumzia Katiba wakati wa kampeni zake kwa hiyo si kipaumbele chake, na kwamba anachotaka kwanza ni “kunyoosha nchi”, kauli inayotafsiriwa kuwa ni kuisigina Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
*Kushughulikia maafa ya Kagera*
Suala jingine ambalo wachambuzi wamelizungumzia ni jinsi Serikali ilivyoshughulikia tetemeko la ardhi lililoikumba mikoa ya Kanda ya Ziwa na hasa, Kagera ambako takribani watu 17 walipoteza maisha, zaidi ya nyumba 840 kubomoka na nyingine 1,264 kuharibika.
Kutokana na janga hilo, Septemba 11, Rais Magufuli aliahirisha ziara ya siku tatu nchini Zambia ambako pamoja na mambo mengine, angehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Edgar Lungu.
Septemba 18 wakati akipokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemeko hilo kutoka kwa Waziri Mkuu, iliyoeleza kuwa zilikusanywa Sh3.6 bilioni, Rais Magufuli alisema Serikali itarekebisha miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko na kuwataka waliobomolewa nyumba, wajipange kuzirekebisha.
Serikali ilizuia watu au taasisi kutoa misaada kwa waathirika, badala yake ikaagiza wapitie Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambaye hivi karibuni alikaririwa akisema kipaumbele itakuwa ni ujenzi wa miundombinu na taasisi za serikali.
*Maamuzi ya haraka*
Serikali inadaiwa kuwajibisha wakuu wa idara kabla tuhuma dhidi yao kuthibitishwa. Baadhi yao walisimamishwa au kufukuzwa kazi katika mikutano ya hadhara na wengine wakati wanaendesha vikao. Jambo hili limekuwa likifanywa hata na wakuu wa mikoa na wilaya kwa kuwaweka mahabusu watu walio chini yao.
*Kuzuia mikutano ya siasa*
Dosari nyingine ni kutofuata Katiba, Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Utumishi wa Umma. Rais amezuia mikutano ya siasa na maandamano. Kwa kuwa Sheria hizo zinaruhusu, Jeshi la Polisi linatekeleza zuio hilo kwa maelezo kwamba ina viashiria vya kuvunja amani au kuibuka kwa magonjwa.
Pia, Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na 1 wa mwaka 1992 uliorudiwa mwaka 2015 umewazuia askari kujihusisha na siasa, lakini wengi wamepewa nyadhifa za siasa.
*Sakata la Zanzibar*
Pia, hali ya kisiasa Zanzibar ni jambo jingine lililozungumzwa na wachambuzi. Wakati akilihutubia Bunge Novemba 20 mwaka jana, Rais Magufuli alionyesha uwezekano wa kuutafutia ufumbuzi mkwamo wa kisiasa Zanzibar na baadaye kuwa na mazungumzo na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad Desemba 21.
Lakini hotuba mbili alizotoa katika ziara ya Pemba Septemba 2 na Unguja Septemba 3, Rais Magufuli aliondoa uwezekano wa kupatanisha makundi hasimu ya kisiasa kati ya CCM na CUF, jambo ambalo limekosolewa na wengi.
“Zanzibar imeathirika sana, yale matumaini ya kuweka mfumo mpya kupitia Katiba Mpya ya Jaji Joseph Warioba yamepotea lakini hata mipango ya kuimarisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa imepotea, “Uchaguzi Zanzibar umeacha mpasuko wa wananchi badala ya kuwaunganisha.” ” – Profesa Abdul Sherrif.
*Matamko ya ghafla*
Jambo jingine lililogusa wengi ni kufuta sherehe za maadhimisho na baadhi katika dakika za mwisho. Mfano ni uamuzi wa kuzuia wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi na maofisa wengine kwenda Simiyu kuhudhuria hafla ya kuzima Mwenge wa Uhuru, wakati baadhi walishafika na wengine wakiwa safarini.
Rais Magufuli aliwaambia maofisa wote waliofika Simiyu au waliokuwa njiani kurudi katika vituo vyao vya kazi na kurejesha fedha walizotumia.
Pia, Rais amekuwa akitoa kauli zinazodaiwa tata ambazo baadhi zinaweza kuwa na madhara kama kuwataka askari wa usalama barabarani kuondoa tairi za gari wanalokamata, au kuwapa polisi fedha za kubrashia viatu.
*Bunge ‘live’*
Suala jingine ni Bunge kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya shughuli za Bunge tofauti na ilivyokuwa katika Bunge la Tisa na la Kumi.
*Kudhibiti mihimili*
Ingawa Serikali ndiyo ina wajibu wa kutafuta fedha, Mahakama na Bunge ni mihimili inayojitegemea. Mwishoni mwa mwaka jana, Rais anadaiwa kuagiza fedha za sherehe ya kuwapongeza wabunge zitumike kununulia vitanda kwa ajili ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), na mapema mwaka huu, aliiomba mahakama imalize kesi za kodi ili Serikali ipate Sh1.4 trilioni na kuupa mhimili huo sehemu ya fedha hizo.
*Mambo mengine*
Mambo mengine ambayo yametajwa kutia doa mwaka mmoja wa Serikali ni nidhamu ya uoga kwa watumishi wa umma pamoja na kuyumba kwa hali ya kifedha miongoni mwa Watanzania jambo ambalo linaonekana kulalalamikiwa na makundi karibu yote.
#MTANZANIA Inaelezwa kutenguliwa kwa mwenyekiti pamoja bodi ya TRA kumesababishwa na kushindwa kutimiza malengo ya serikali kukusanya mapato pic.twitter.com/o5tTa3vyky
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MAJIRA Vijana walioathirika na dawa za kulevya ktk kituo cha Souber House Kigamboni wamesema wako tayari kutaja majina ya wauzaji wakubwa pic.twitter.com/jO5ToHVc2V
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#Jukwaa la Katiba Tanzania JUKATA wamemuomba Rais JPM aendeleza mchakato wa katiba mpya ambao upo katika ilani ya chama cha mapinduzi CCM pic.twitter.com/cUxNxEcLWc
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MAJIRA Jeshi la polisi mkoani Tanga limetangaza dau kwa atakayefanikisha kukamatwa askari wake Michael Kombo aliyemuua mwenzie kisa mapenzi pic.twitter.com/7g619zBpS1
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MAJIRA Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda Padri Kasomo ametaka watu waache tabia ya kuzaa watoto wengi na kushindwa kuwatunza pic.twitter.com/NANJRfiqzy
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#HABARILEO Serikali imesema inaangalia uwezekano wa moja ya sifa za halmshauri iwe ni kuwa na gari la zima moto ili kukabiliana na majanga pic.twitter.com/j4pQDzOpDI
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#HABARILEO Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Kilimanjaro imeshangazwa juu ya taarifa za wanafunzi wa3 wa sekondari kupewa mimba na wazazi wao pic.twitter.com/XMWgQTxjav
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#HABARILEO Serikali imezitaka familia kukataa kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili jambo linalosababisha watoto wao kukimbia majumbani pic.twitter.com/Z9Ukpripym
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#HABARILEO Mtu mmoja kati ya watatu kutoka Manispaa ya Iringa inaelezwa hana uelewa wa matumizi sahihi ya choo pic.twitter.com/CEB4WSLc1Y
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#HABARILEO Club ya Manchester City iko tayari kuvunja benki ili kumsajili nyota Lionel Messi kwa ada ya pauni mil. 200 zaidi ya Tsh Bil. 500 pic.twitter.com/bBo00YHwLH
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MTANZANIA Walalamikaji katika kesi ya kupinga ubunge wa Ester Bulaya CHADEMA, ktk jimbo la bunda wamesema watakata rufaa juu ya hukumu hiyo pic.twitter.com/d221YQ6PxK
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MTANZANIA Mshambuliaji wa club ya Newcastle Dwight Gayle anadaiwa kutolewa meno na watu wasiojulikana baada ya kumvamia usiku wa maneno pic.twitter.com/o41hFQpG7O
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MWANANCHI Unafiki,Majungu, Rasilimali za Chama, Mfumo mbovu wa kupata viongozi, kutolinda haki za wanachama vimetajwa na Bashe kuitesa CCM pic.twitter.com/SSlE72JoRv
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MWANANCHI Mbunge mstaafu James Lembeli amesema Rais John Magufuli hatafanikiwa vita ya ujangili kutokana na kuzungukwa na wanaowasaulidia pic.twitter.com/BH0T1Jcgka
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
#MWANANCHI Mzee wa miaka 90 nchini Canada amejichimbia Kaburi licha ya kuwa mzima kiafya na kudai anajivunia kuchimba kaburi kabla hajafa pic.twitter.com/JxQYtHx44s
— millardayo (@millardayo) November 21, 2016
VIDEO: Alice Tupa anakuchambulia Magazeti yote ya leo November 21, 2016 kuanzia Hard News, mpaka Sports. Tazama hapa chini.