Usiku wa January 22 2017 michezo ya mwisho ya Kundi A ya michuano ya mataifa ya Afika 2017 maarufu kama AFCON, ilichezwa kwa muda mmoja kuepusha upangaji wa matokeo kutokana na timu zote nne kuwa na nafasi ya kusonga mbele.
Kwa bahati mbaya AFCON 2017 imeshuhudia mwenyeji Gabon akiaga mashindano hayo kutokana na kulazimishwa sare tasa na timu ya taifa ya Cameroon, hiyo inakuwa sare ya tatu kwa Gabon ambapo sare hiyo imewafanya wafikishe point tatu na kuambulia kushika nafasi ya tatu huku Guinea Bissau wakishika mkia.
Cameroon na Burkinafaso wao wanatinga moja kwa moja robo fainali ya AFCON kufuatia kufikisha point 5 kila mmoja, Burkinafaso anafuzu baada ya kuifunga Guinea Bissau kwa goli 2-0 katika mchezo wa leo, hivyo wapo nafasi ya kwanza wakiwa na point 5 sawa na Cameroon lakini wanaongoza kwa tofauti ya magoli.
Msimamo wa Kundi A #AFCON2017 umemalizika hivi kwa Burkinafaso na Cameroon kutinga robo fainali. pic.twitter.com/CuNsxFj5si
— millard ayo (@millardayo) January 22, 2017
https://youtu.be/gbaVx7NJ9Ak
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4