Baada ya siku mbili za mapumziko kutokana na kumalizika kwa hatua ya makundi ya michuano ya AFCON 2017, January 28 michezo miwili ya robo fainali ilichezwa katika uwanja wa Amitie na Franceville, game ya kwanza ya Burkinafaso walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Tunisia.
Game ya pili ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka sehemu mbalimbali hususani wa Liverpool, wamuone staa wao Sadio Mane akiiongoza Senegal kupambana dhidi ya Cameroon ilipigwa Franceville na kujikuta Senegal wakiondolewa katika michuano hiyo kwa penati 4-5.
Sadio Mane ambaye ni moja kati ya wachezaji ghali wanaotokea Afrika ameshindwa kuibeba Senegal baada ya kujikuta penati yake ya tano ikiishia mikononi mwa golikipa wa Cameroon Fabrice Ondoa, kabla ya Vincent Aboubakar kuifungia Cameroon penati ya tano na ya ushindi.
Mikwaju ya penati ililazimika kupigwa baada ya dakika 120 za mchezo kumalizika pasipokufungana, ushindi huo unaifanya Cameroon kucheza na mshindi wa mchezo wa Misri vs Morocco nusu fainali, hii sasa inakuwa ni mara ya 5 kwa Senegal kuondolewa katika michuano ya robo fainali ya AFCON kati ya mara 7.
https://youtu.be/KWo2TpJsIBA
VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4