Kuelekea siku ya Wapendanao ‘Valentine Day’ staa kutoka Bongo movie Irene Uwoya ameamua kutengeneza utaratibu wa kila siku kutaja kitu ambacho tulikua hatukijui kuhusu yeye ambapo leo February 8 2017 ameanza kwa kutupia moja.
Pamoja na urembo alionao Irene Uwoya kumbe hazimiki au hashtuki anapoona vijana wenye mionekano mizuri yaani ‘Handsome Boy’ na anasisitiza >>’Kitu ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa SIJAWAHI kuvutiwa na Wanaume wenye mionekano mizuri‘
‘Sielewi ni kwanini lakini wanaume wenye sura mbaya huwa wanaamsha hisia zangu za KIMAPENZI‘ – Irene Uwoya.
Uliiona hii ya Msami kutoa sababu za kuachana na Irene Uwoya? bonyeza play hapa chini kutazama alichosema