Imeripotiwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa kuwa Mrithi wa kampuni kubwa ya vifaa vya Elektroniki ya Korea Kusini Samsung Lee Jae-Yong amekamatwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi kuhusu kesi ya kuondolewa madarakani rais wa taifa hilo Park Guen-Hye.
Miongoni mwa mengine, anatuhumiwa kuhusika katika ufisadi ambapo Mwendesha mashtaka amesema Lee Jae-yong alilipa zaidi ya dola 35 milioni za Marekani zinazoungwa mkono na Choi Soon-sil, rafiki wa Rais Park Geun-hye.
Mwendesha mashtaka huyo anasema pesa hizo zilikusudiwa kuhakikishia uungwaji mkono wa mpango wa kuunganisha kampuni mbili zilizohusishwa na Samsung ambapo Ijumaa, Mahakama ilisema kwamba ilikuwa imekubali akamatwe kutokana na mashtaka yaliyoongezwa na ushahidi mpya uliopatikana.
Kwa sasa ni Naibu mwenyekiti wa Samsung Electronics lakini tangu baba yake, Lee Kun-hee alipopata mshtuko wa moyo mwaka 2014, amekuwa akitazamwa kama mkuu wa kampuni hiyo.
Kashfa hiyo inatishia kumtoa madarakani rais wa taifa hilo Park Guen-Hye ambaye kwa sasa amesimamishwa kazi kwa muda wakati Mahakama ya juu inapoendelea kuchunguza tuhuma dhidi yake na mswada wa kumuondoa madarakani.
AyoTVMAGAZETI: Polisi yanawa mikono askari tisa wa Makonda, Vituo 155 vya QT kufutwa, Bonyeza play hapa chini