Mrembo kutoka Tanzania Jokate sasa hivi yuko Marekani ambako ameongozana na Team ya Basketball inayohusika na ishu za mpira wa kikapu kutoka Afrika (NBA Africa) yenye makao makuu yake Johanesburg, Afrika Kusini.
Jokate ameiambia millardayo.com kwanini alipata nafasi ya kuhudhuria tukio kubwa la NBA All Star Weekend ambapo amesema kuwa ni kutokana na project zake za kujenga viwanja vya michezo kwenye mashule na vyuoni, yeye na Team yake wamepata nafasi ya kutangaza game ya NBA Africa ambayo itafanyika August 5, 2017 Johannesburg, Afrika Kusini.
Pia amekutana na mastaa wakubwa wa muziki kutoka Marekani akiwemo Jay Z na mkewe Beyonce, Akon, Jidenna, Remmy Ma na wengine wengi na hakuogopa kwenda kuwasalimia Beyonce na Jay Z pamoja na ulinzi mkubwa walionao >>> “Nilienda tu kuwasalimia kwasababu nawapenda ikawa bahati yangu nikafanikiwa wengine walishindwa” – Jokate
Kwa mujibu wa Jokate, amesema kupitia NBA Africa tayari kuna mastaa wa Basketball watano Pascal Siakam, Thon Maker, Cheick Dialo, Abdel Nader na Ben Bentil wameingizwa kwenye ligi ya Chama Cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA).
“Mimi kupitia project zangu za kujenga viwanja vya michezo wakaona kama mdau na influencer naweza kuungana nao kusambaza hii habari na pia kutoa hamasa nikaungana na akina Akon, Jidenna”. – Jokate
VIDEO: Kutana na Mwigizaji Tanasha, video Queen wa ‘nagharamia‘ ya Alikiba na Christian Bella, bonyeza play kwenye hii video hapa chini
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo