Baada ya sauti zilizosambaa zikimuhusisha Mwigizaji Steve Nyerere na Mama wa mwigizaji Wema Sepetu wakizungumza huku akitaja baadhi ya viongozi mbalimbali aliodili nao kwenye sakata la Wema kushikwa na Polisi, leo Steve Nyerere ameita Waandishi wa habari na kuongea nao.
Wakati ukiisubiria FULL VIDEO kwenye Youtube ya “millardayo“, hizi kwenye Tweets za ‘millardayo‘ hapa chini ni kauli za Steve Nyerere.
"Nimewaiteni hapa kama msanii wa tasnia ya filamu pia kama kada wa chama cha mapinduzi"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
'Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Nilichofanya ni kutumia sanaa yangu na ujuzi kumtoa mama kwenye hali ambayo anasema anataka kujitoa hata kwenye chama"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Mama alikuwa anaamini naweza kumtoa Wema, nilikuwa natumia ujuzi wa akili yangu kumlidhisha mama, kumbe yeye ananirekodi"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Kwenye kampeni tulilipwa hakuna aliyefanya kazi bila kulipwa, kundi la mama ongea na mwanao mimi ndio nilikuwa mwenyekiti"Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Maneno niliyoyasema ktk simu na Mama Wema na kutaja viongozi ni UONGO, ilibidi nifanye hivyo maana sikuwa na jinsi…" – Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Uwezo wa kuwaambia Wabunge au kuwaelekeza cha kufanya sina, sina ujanja huo…. namuomba radhi Spika Job Ndugai" -Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Mimi na Wema ndio tuliwafuata CCM kwamba tuna wazo la mama ongea na mwanao, na tukalipwa"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Nia yangu haikua mbaya, wakati naongea na Mama niliamini ni mama mzazi… ile audio ina siku 5, kwanini iachiwe juzi?"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"fikifria ile audio ina siku tano, inakuja kutolewa juzi na watu wamehama tayari chama, nafikiri walifanya hivyo kunichafua"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Ile audio imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi" – Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Nimetaja viongozi ktk ile audio alafu unakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya kuisambaza ni mauaji" – Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Si kweli nilishinkiza wabunge wamjadili Wema, mtoto anapotaka kuchomwa Sindano kuna vitu anaambiwa, ndio hivyo nilivifanya;-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Watanzania wenzangu usimuamini binadamu yeyote, Mama Wema alitaka kuniharibia maisha yangu, Mama kanikosea.. namuachia Mungu"-STEVE NYERERE
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Mimi na Makonda hatujawahi kwenda alikokutaja Mama, ilibidi niitikie kama zoba, Waandishi naomba mkaseme NAOMBA RADHIII" – Steven Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Sina ugomvi na Makonda na ninamuomba msamaha na hakuna ukweli kwamba siongei nae…. Paul ni kaka yangu, tunawasiliana" – Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Naliomba radhi bunge tukufu na Spika Ndugai kwa kauli ya kusema nimeshinikiza bunge, nilifanya hivyo kutaka asitoke ndani ya CCM"-Steve
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Uwezo wa kuwashinikiza wabunge sina na wala mamlaka hiyo sina"-Steve Nyere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Hii kesi kila mtu alirudi nyuma.. ni maulizo tu inaendeleaje? tunamuombea kwa Mungu tu, CCM ni kama bahari wametoka wangapi?"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Mimi kama mtu wa karibu na familia nilitakiwa nitoe maneno matamu na ndio hayo"-Steve Nyerere
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Kwenye project ya kampeni ya uchaguzi mkuu 2015 MAMA ONGEA NA MWANAO hatuidai CCM hata senti tano" – Steve Nyerere #MillardAyoUPDATES
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
"Alichofanya mama kunirekodi huo ni uuaji, kuna watu wananitegema nyuma ya Steve alitaka anigombanishe na marafiki"-Steve Nyerere.
— millardayo (@millardayo) February 25, 2017
VIDEO; Mama Wema kuhusu simu ya Steven Nyerere na kuhamia CHADEMA, Bonyeza Play hapa chini
FULL VIDEO: Wema Sepetu alivyotangaza kuhamia CHADEMA, bonyeza play kwenye hii video hapa chini kujionea
EXCLUSIVE: Yvonne Chakachaka alivyomuongelea Alikiba, TAZAMA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI