Usiku wa March 3 2017 mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea ambaye kwa sasa anaichezea Atletico Madrid ya kwao Hispania Fernando Torres, jina lake lilitawala mitandaoni baada ya kugongwa na kupoteza fahamu uwanjani wakati wa mchezo dhidi ya Deportivo La Coruna.
Good news ikufikie kuwa Fernando Torres anaendelea poa na aliruhusiwa kutoka hospitali asubuhi ya March 3, lakini leo Torres ameonekana akihudhuria katika uwanja wao wa nyumbani wa Vicente Calderon kuangalia timu yake ikicheza dhidi ya Valencia.
Kuonekana kwa Torres uwanjani mbele ya mashabiki akiwa jukwaani kulileta furaha kwa mashabiki wa soka na kujua kuwa anaendelea vizuri na jeraha lake la kichwa, Torres aliishuhudia timu yake ikiifunga Valencia goli 3-0.
ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2