Leo March 7 2017 imeripotiwa taarifa za msiba kutoka kwenye familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete ambapo imeelezwa Bibi Nuru Halfani Kikwete ndie aliyefariki usiku wa kuamkia leo akitibiwa kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ndugu wapendwa, nawashukuru sana kwa salamu za pole na upendo kufuatia kifo cha Mama yangu mdogo mpendwa Bi Nuru binti Halfani Shomvi. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mama amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mama yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
Mama yetu mdogo aliitwa jana na Mola, na kuitika. Shughuli za msiba ziko nyumbani kwa marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7, 2017
VIDEO: Simu ya Mzee Kikwete aliyompigia Ridhiwani baada ya kuona picha yake na Lowassa? Bonyeza play hapa chini kutazama
UNAZITAKA ZOTE BREAKING NEWS NA MATUKIO YA HABARI, PICHA NA VIDEO ??? ungana na Reporter wako Millard Ayo kwenye mitandao yote ya kijamii na utapata yote yanayonifikia saa 24… BONYEZA HAPA >>> Twitter Facebook Instagram