Usiku wa April 11 2017 mchezo wa robo fainali ya UEFA Champions League kati ya Borussia Dortmund dhidi ya Monaco uliahirishwa kwa sababu za kiusalama, hiyo inatokana na Borussia Dortmund kushambuliwa saa chache wakiwa wanaelekea uwanjani kwa ajili ya game hiyo.
Tukio hilo la shambulio lilitokea Ujerumani kwa mujibu wa mtandao wa BBC News imeripoti kuwa shambulizi hilo linahusishwa na kikundi cha Islamist kutoka Syria na mchezaji Marc Bartra ndio mchezaji pekee wa Dortmund aliyeumia katika tukio hilo na amefanyiwa upasuaji.
Marc Bartra alifanyiwa upasuaji wa mkono wake usiku wa April 11 baada ya kuvunjika mfupa kutokana na tukio hilo, Marc Bartra mwenye umri wa miaka 26 amekuwa mchezaji muhimu wa Dortmund akiwa kaichezea timu hiyo katika michezo 30.
VIDEO: Simba imekubali kipigo cha nne cha VPL vs Kagera April 2 2017