Mpaka 2013 imemalizika, Kiswahili kimechukua headlines mara kadhaa kwenye AyoTV na millardayo.com kutokana na kutumika kwenye sehemu ambazo hatujazoea kuona kikitumika mfano kupatikana kwa video za raia wa Marekani na nchi nyingine za Ulaya wakiimba Bongoflevana kuzungumza Kiswahili darasani.
Wakati kilipotokea kifo cha mzee Nelson Mandela, staa wa hiphop duniani Nicki Minaj alimiliki headlines kwenye nchi zinazoongea Kiswahili baada ya kuandika ujumbe kuhusu mzee Mandela na kisha kumalizia kwa kuandika kiswahili ‘madaraka kwa wote’ kwenye page yake ya Instagram.
December 31 2013 saa kadhaa kabla ya kuumaliza mwaka staa wa hiphop kutoka Marekani pia ambae jina lake lina neno la Kiswahili Talib Kweli (38), aliweka neno la Kiswahili kwenye moja ya sentensi zake ndani ya mtandao wa twitter alio na wafuasi zaidi ya laki nane huku akiwa anafatwa na mastaa kadhaa wa bongo akiwemo Nikki wa II, Godzilla, Profesa Jay, Chidi Benz, Fid Q, Vanessa Mdee na wengine.