Kila inapoingia siku mpya, binadamu amekuwa akifikiria mbinu mpya ambayo itamsaidia katika maisha yake ya kila siku, na kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kugundua vitu vipya imekuwa rahisi sana kwa binadamu.
Leo April 18, 2017 nimekutana na stori unayohusu kifaa maalum kilichotengenezwa nchini Japan ambacho kitatumika kuscan na kuweka kwenye begi lako bidhaa zozote utakazonunua kwenye supermarkets.
Daily Mail imeripoti April 18, 2017 kuwa kifaa hicho kinachoitwa Reji Robo kimetengenezwa na kampuni ya Panasonic ikiwa ni mfumo maalum kwa ajili ya kuscan ili kuokoa muda wa manunuzi ambapo hutumia radio-frequency ID ambayo imewekwa katika kila bidhaa huku wanachotakiwa kufanya wanunuzi ni kuchagua bidhaa wazitakazo kisha wanasogeza vikapu vyao sehemu ya kuscan, halafu kifaa hicho hufanya kazi iliyobaki.
Kwa mujibu wa website ya Japan ya Nikkei Asian Review Reji Robo inatumika katika baadhi ya maduka ya Japan lakini lengo kubwa ni kutumika nchi nzima ifikapo mwishoni mwa 2025 huku kampuni iliyoratibu mfumo huo Panasonic ikidai kuwa teknolojia hiyo itapunguza muda wa kufanya manunuzi kwa 10%.
Nimekuwekea video hapa chini bonyeza play kutazama…
VIDEO: Zikufikie taarifa za kifo cha baba yake staa wa Bongofleva Belle 9. Bonyeza play kutazama.