Baada ya kuwepo kwa taarifa za zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu thamani halisi ya hisa za Vodacom (VTL), Kampuni ya Vodacom Tanzania wametolea ufafanuzi. Moja ya ujumbe uliosambazwa April 19 2017 umedai kuwa bei ya TZS 850 kwa hisa ni mara 3.8 zaidi ya thamani halisi ya hisa hizi.
Taarifa iliyotolewa na kampuni ya Orbit Securities Ltd imedai kuwa njia iliyotumiwa na mwandishi aliyekokotoa thamani ya vitabuni ya rasilimali za kampuni, akatoa dhima (madeni) na kudai kuwa aliyobaki ndiyo thamani halisi ya hisa za wamiliki wote wa kampuni ni potofu na inaonyesha ni kwa kiwango gani mwandishi haelewi jinsi thamani za hisa na kampuni zinavyokokotolewa.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mwandishi anadai kuwa ukweli kwamba bei ya toleo ya hisa za VTL ya TZS 850, sawa na mara 3.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali kujitoa dhima, ni ushahidi kuwa bei imewekwa ya juu sana lakini siku hiyo hiyo, bei ya hisa za Safaricom katika soko la hisa la Nairobi ilikuwa ni mara 5.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali baada ya kutoa dhima.
VIDEO: Kama una mpango wa kununua hisa za Vodacom, kuna hii Good News, Bonyeza play hapa chini kutazama