Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametoa agizo la kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Castory Manase Nkuli baada ya kudaiwa kunyang’anya ardhi ya vijiji na kumilikisha kampuni.
Castory Manase Nkuli anadaiwa kuchukua ardhi ya ukubwa wa ekari 4,000 ya vijiji vya Ruvu na Mchinga na kuimilikisha kwa kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi. Immaculate Senje amesema kuwa utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wanakijiji.
Nimekuwekea full video hapa chini, bonyeza play kutazama…
VIDEO: TAKUKURU imezitaja taasisi zinazoongoza kwa rushwa. Bonyeza play kutazama…