Siku moja baada ya Ligi Kuu soka Tanzania bara inayoandaliwa na kusimamiwa na shirikisho la soka Tanzania TFF kumalizika kwa Yanga kupata Ubingwa wa Ligi hiyo kwa tofauti ya magoli 10 baada ya kufungana kwa point 68 sawa na Simba.
Simba wao baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui uliyochezwa uwanja wa Taifa na kumalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Mwadui FC, ilitangazwa kuwa wangepewa zawadi ya medali ya mshindi wa pili wakiwa uwanjani hapo lakini game ilipomalizika waliingia vyumba vya kubadilishia nguo na kutotoka.
Kitendo ambacho kimetafsiriwa ni sawa na kugomea medali hizo kutokana na kuwa bado hawaikubali nafasi waliyopo hadi malalamiko yao ya kuzidai point 3 dhidi ya Kagera Sugar yatakapofanyiwa ufumbuzi na FIFA, AyoTV imempata afisa habari wa TFF Alfred Lucas aeleze kanuni zikoje kuhusu kitendo hicho.
“Tunaamini mpira wa miguu ni mchezo wa kiungwana ndio maana kaulimbiu ya FIFA inasema football is the game of fair play ndio maana linapofanyika jambo si la kiungwana tunarudi katika kanuni, VPL inamtambua mshindi wa kwanza, pili, watatu na nne sasa inapotokea unagomea zawadi kama una maelezeo hayana hoja kuna adhabu” >>>Alfred