May 20 2017 Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 ulimalizika rasmi kwa michezo nane kuchezwa kwa mara moja ili kuepusha kupangwa kwa matokeo ya mechi hizo, Yanga ambao walikuwa wanatetea Ubingwa wao walikuwa jiji Mwanza kucheza dhidi ya Mbao FC.
Mchezo wa Yanga dhidi ya Mbao FC licha ya kuwa Yanga alikuwa tayari ana asilimia 99 ya kutwaa taji hilo kutokana na kuwa na magoli mengi zaidi ya Simba aliyekuwa anamfuatia ilimalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0 lakini ametangazwa Bingwa kwa kuizidi Simba magoli 10 licha ya wote kuwa na point 68.
Ubingwa wa Ligi Kuu wa Yanga unakuwa ni Ubingwa wao wa tatu mfululizo wa Ligi Kuu lakini ni Ubingwa wao wa 27 wa Ligi Kuu kwa muda wote, wakati watani zao Simba wao wanakuwa hawajawahi kutwaa taji hilo kwa misimu minne mfululizo, timu za African Lyon, Toto na JKT Ruvu zimeshuka daraja na nafasi zao zitazibwa na Singida United, Njombe na Lipuli FC zikipanda
Msimamo wa VPL umemalizika hivi Yanga akiwa Bingwa kwa tofauti ya magoli 10 A.Lyon, Ruvu JKT na Toto zimeshuka daraja #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/4fiLyemjvH
— millard ayo (@millardayo) May 20, 2017
VIDEO: Tazama hapa chini mazoezi ya Serengeti Boys wakiwa Gabon