Siku moja baada ya tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kufanyika na kutoa zawadi kwa wahusika huku timu ya Simba ambayo ni mshindi wa pili kutokuwepo wala kutuma muhusika katika eneo la tukio ikihisiwa kuwa ni muendelezo wa kugomea zawadi ya mshindi wa pili.
Leo May 25 2017 ziliripotiwa habari za uongo katika mitandao ya kijamii kuwa wekundu wa Msimbazi Simba kupitia kwa Rais wao Evans Aveva wamekubali nafasi ya mshindi wa pili na kufuta malalamiko yao FIFA kuhusiana na TFF kuituhumu kutotenda haki.
Uongozi wa Simba SC kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii zimekanusha taarifa hii iliyokuwa inasambaa mtandaoni #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/QyEIwSly5U
— millard ayo (@millardayo) May 25, 2017
Simba imekanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wao wa instagram “Wanachama, wapenzi na mashabiki wa Simba Sports Club tunawaomba mpuuze ujumbe huu unaosambazwa. Uongozi wa Simba haujatoa taarifa hii”
Unaweza kutazama mahojiano ya Mkurugenzi wa SportPesa na AyoTV baada ya kuingia mkataba.