Mwili wa mzee Francis Maige Kanyasu maarufu kama Ngosha unatarajia kuagwa June 3, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupatikana ndugu zake.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya imeeleza kuwa mwili huo utaagwa majira ya saa 2:30 Asubuhi katika Hospitali hiyo na utasafirishwa hadi kijijini kwao Igokero, Misungwi Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Mzee Francis ambaye alichora Nembo ya Taifa alifariki Usiku wa May 29, 2017 akiwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na umri wa miaka 86.
Serikali imesema mwili wa "Ngosha" aliyeshiriki kuchora Nembo ya Taifa utaagwa Muhimbili Hosp. na kusafirishwa kwenda Misungwi kwa Mazishi. pic.twitter.com/3GRPYIE6IW
— millardayo (@millardayo) June 2, 2017
Profesa UDSM kuhusu aliyechora Nembo ya Taifa