Staa wa soka wa Kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo licha ya kutetewa na club yake ya Real Madrid kuhusiana na tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili, ameripotiwa kufikiria kufanya maamuzi magumu.
Cristiano Ronaldo ambaye ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Real Madrid anatuhumiwa kukwepa kodi nchini Hispania katika kipindi kati ya 2011 hadi 2014 kiasi kinachotajwa kufikia pound milioni 13 ambazo ni zaidi ya Bilioni 35 za kitanzania.
Mtandao wa Sky Sports umeripoti kuwa staa huyo aliyeisaidia Real Madrid kutwaa mataji matatu ya UEFA Champions League anataka kuondoka Hispania kutokana na tuhuma zinazoendelea ambazo anaamini hafanyiwi haki.
Kama kuna timu itakuwa inamuhitaji Cristiano Ronaldo kumtoa Hispania na kumsajili katika timu yao basi italazimika kuilipa Real Madrid euro bilioni 1 ambazo ni zaidi ya trilion 2.5 za kitanzania, hiyo ni kwa mujibu wa kipengele kilichopoa katika mkataba wake na Real Madrid.
BREAKING: @Cristiano wants to leave @realmadrid because he does not want to play in Spain any more – Sky sources. #SSNHQ pic.twitter.com/wic48f13uL
— Sky Sports News HQ (@SkySportsNewsHQ) June 16, 2017
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera