Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo June 28, 2017 amekutana na Waandishi wa Habari DSM kuzungumzia mustakabali wa Chama akisema Msajili wa Vyama vya Siasa anaihujumu CUF kwa kutumia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).
Haya hapa mambo makubwa 14 Maalim Seif ameyazungumza kuhusu Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini RITA na Mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili Prof. Lipumba.
"Sisi hatutovunjika moyo na maamuzi yoyote ya mahakama, sisi tuko makini, fujo hatutaki lakini tunataka kufuata sheria za nchi"-Maalim Seif pic.twitter.com/62YBvaKwOw
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Hakuna upande wa Lipumba na Maalim Seif bali ni mgogoro kati ya Lipumba, kikundi chake na Chama cha CUF, chama sio cha mtu"-Maalim Seif pic.twitter.com/hnL6HULbIb
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Msajili wa vyama vya siasa tunamshtaki kwa kuiba pesa zetu ndio maana anatafuta kesi ifutwe"-Maalim Seif pic.twitter.com/rvVTe70ZvZ
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Naamini hapa tulipofika ni mwenyezi Mungu tu anaweza kuzuia haki isipatikane na si mwingine"-Maalim Seif pic.twitter.com/ZdLSwE6TDu
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Kwa nini nasema bodi ya Lipumba ni feki, ni kwa sababu katiba ya CUF mamlaka ya kuteua ipo chini ya baraza kuu, msajili anajua-Maalim Seif pic.twitter.com/V6MvKGUSRM
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Sisi tunaona chombo kinachoweza kurejesha haki ni mahakama hata kama itachelewa, haki haipotei"-Maalim Seif pic.twitter.com/bVxEwZQKJU
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Lipumba si mwanachama na hawezi kuwa mwenyekiti, sisi tunasema ni mwenyekiti wa msajili"-Maalim Seif pic.twitter.com/b9IvpfiAp4
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Nikae na Lipumba kama nani? Lipumba alijiuzulu mwenyewe kwa utashi wake na barua iliwasilishwa kwenye mkutano mkuu wa Taifa"-Maalim Seif pic.twitter.com/LGgVktBIg0
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Chama cha CUF kimepata mshtuko mkubwa sana baada ya kuona taasisi kubwa (RITA) inaghushi nyaraka"-Maalim Seif pic.twitter.com/gJkFrNKOsD
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Taarifa za kusajiliwa kwa bodi feki ya Prof. Lipumba zilipatikana June 20 2017"-Maalim Seif pic.twitter.com/MnlCE0g7ha
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Wamesajili bodi feki ili kufuta kesi zote zilizosajiliwa, kufungua akaunti benki na
Kumuondoa madarakani katibu Mkuu"- Maalim Seif pic.twitter.com/t7dBShMee4
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"RITA walikubali ombi la msajili wa vyama vya siasa, wameghushi mpaka sahihi ya Lipumba licha ya kwamba ni mshiriki wao"-Maalim Seif pic.twitter.com/oT6hgFE1Z7
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Msajili wa vyama vya siasa aliwasiliana na RITA akiomba kusaidiwa kughushi kumbukumbu za bodi ya CUF"-Maalim Seif pic.twitter.com/kFoqoVe5Qw
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
"Tunazo taarifa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA ameshinikizwa kuandisha wajumbe feki wa bodi ya CUF"- Maalim Seif pic.twitter.com/cPoy9bs6PR
— millardayo (@millardayo) June 28, 2017
FULL VIDEO: Maalim Seif amekutana na Waandishi wa Habari leo DSM na kuzungumza nao huku akiituhumu RITA na Msajili wa Vyaa vya Siasa kwa kusema kuwa wanaihujumu CUF…hii hapa FULL VIDEO unaweza kuitazama kwa kubonyeza PLAY!!!