Kama kawaida millardayo.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku kupitia twitter account @millardayo na leo July 14, 2017 pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali ya Tanzania.
Chukua muda wako kupitia kila udondozi wa kilichoandikwa kwenye magazeti hayo.
TAKUKURU imesema wakurugenzi, mameneja 12 walioachishwa kazi na NSSF wanachunguzwa na wakati wowote hatua za kisheria zitachukuliwa #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Mahakama Kuu Kanda ya Moshi imeanza kusikiliza kesi inayomkabili DC Gelasius Byakanwa iliyofungiliwa na Kilimanjaro Veggies Ltd. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amevionya vyama vya Wananchi CUF na CHADEMA akivitaka kuacha kutishana. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar 'SMZ', imesema wananchi wanatakiwa kuacha mtazamo hasi kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
"Wenye vyeti darasa la saba wataendelea kuwa watumishi wa umma katika vyeo vyao." – Dk. Laurean Ndumbaro. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Waajiri wametakiwa kufanya uhakiki wa kina wa vyeti kwa ajira mpya zitakazotolewa ili kuwa na watumishi wa umma wenye sifa. #MAJIRA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amepewa saa 168 za kuripoti katika Ofisi za Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, DSM. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Serikali za Tanzania na Uganda zimetiliana saini ya makubaliano ya kusafirisha mizigo kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Serikali imesema wakati ipo ktk hatua za mwisho kutoa ajira mpya 62,000 ifahamike hakuna ajira itakayotolewa bila uhakiki wa vyeti. #UHURU.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
IGP Sirro amemteua Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Fortunatus Musilimu kuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa Forodha na Ushuru wa TRA Tiagi Masamaki na wenzake. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Acacia, Balozi Juma Mwapachu amestaafu nafasi hiyo baada ya kutumikia kwa vipindi viwili. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Serikali imesema kukamilika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa 'standard gauge' kutasaidia kuboresha mfumo wa usafirishaji. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Sahara Media Group inayomiliki Star TV, RFA na Kiss FM imo hatarini kupigwa mnada ikidaiwa kodi ya Tsh. bil 4.5 na TRA. #TanzaniaDAIMA.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Magunia 428 ya bangi na 6 ya mbegu za bangi yamekamatwa katika kitongoji cha Longong, Engalaoni, Arumeru usiku wa kuamkia jana. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
CHADEMA Kanda ya Kaskazini imekishutumu @ccm_tanzania kuwa kinatumia fedha kuwashawishi madiwani na wenyeviti wahame chama chao. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Mwanamke mkazi wa Chamwino, Dodoma ametaka haki itendeke baada ya kubakwa na mbakaji kufungwa jela miezi 6 au faini ya 300,000. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Serikali imetangaza watumishi wa umma 450 wameshinda rufaa kati ya 1,050 waliokata rufaa baada ya kutajwa ktk list ya vyeti feki. #HabariLEO
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Jeshi la Polisi limethibitisha aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga ameteuliwa kuwa RPC Mbeya. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald 'Masogange' hajasikilizwa kutokana na mshtakiwa kudai anaumwa. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Naibu Waziri wa Nishati ametoa siku 13 kwa mameneja wa Tanesco kuhakikisha wananchi waliolipa ada wanaunganishiwa haraka umeme. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
TRA imeanza kuchukua hatua ya kuvifungia vituo vyote vya mafuta ambavyo pampu zake hazijafungwa moja kwa moja na mashine za EFD. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 14, 2017
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Laurean Ndumbalo amezungumza kuhusu Watumishi wa Umma ambao hawajawasilisha vyeti vyao vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne na kidato cha sita kwa ajili ya kuahakikiwa na baraza la mitihani Tanzania…bonyeza PLAY kwenye VIDEO hii kutazama zaidi.
Bonyeza PLAY kwenye VIDEO hii hapa chini kuna GOOD NEWS iliyoelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Laurean Ndumbalo kuhusu nafasi za kazi 10,184 ambazo vibali vyake wameanza kuvitoa na mwezi ujao nafasi zitatangazwa.